EAC yasema Uganda itaendesha kongamano la 11 la utawala wa mtandao wa internet wa Afrika Mashariki
2024-07-16 09:34:48| CRI

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jumatatu ilitoa taarifa mjini Arusha nchini Tanzania ikisema Uganda itaendesha kongamano la 11 la utawala wa mtandao wa internet la Afrika Mashariki (EAIGF), ili kutatua masuala makuu ambayo yataongeza maendeleo na utawala wa mtandao wa internet kwenye kanda hiyo.

Taarifa hiyo ilisema EAC ikishirikiana na tawi la Shirikisho la Jamii ya Mtandao wa Internet la Uganda, wataendesha kongamano la “Kujenga Mustakabali wa Wadau mbalimbali wa Kidigitali wa Afrika Mashariki” mjini Kampala kuanzia tarehe 11 hadi 12 Septemba.

Naibu katibu mkuu wa EAC anayeshughulikia sekta za miundombinu, uzalishaji, jamii na siasa Andrea Aguer Ariik Malueth alitoa wito kwa wahusika wa sekta ya TEHAMA na wadau wengine kutumia kongamano hilo ili kuweka agenda ya mafungamano ya kidigitali kwa ajili ya kanda hiyo.