Matokeo ya awali ya kura zilizohesabiwa yaonesha Kagame anaongoza kwa asilimia 99.15
2024-07-16 09:36:13| CRI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda imesema kwa mujibu wa matokeo ya awali ya asilimia 79 ya kura zilizohesabiwa, rais wa sasa wa Rwanda Paul Kagame anaongoza kwa asilimia 99.15 ya kura katika uchaguzi wa rais uliofanyika siku ya Jumatatu.