"Tuna matumaini kuwa uchumi wa China utaendelea kukua katika muda mrefu. Tunaamini kwamba sera nyingi zaidi zitahakikisha ukuaji wa uchumi, kampuni yetu pia itastawi zaidi." Tarehe 15, baada ya China kutoa rasmi takwimu za uchumi wa taifa kwa nusu ya kwanza ya mwaka, Wang Mingzhi, makamu meneja mkuu wa kampuni ya OSIM ya Singapore alitoa maoni hayo.
Takwimu zinaonesha kuwa, pato la taifa katika nusu ya kwanza ya 2024 lilifikia yuan bilioni 61,683.6, ambalo liliongezeka kwa asilimia 5.0.
Makamu wa rais wa utafiti na mikakati katika Chuo Kikuu cha Biashara ya Kimataifa na Uchumi cha Israeli, amesema hatua ya China kuondoa vikwazo zaidi vya uwekezaji wa kigeni katika sekta yake ya viwanda itawezesha ufunguaji mlango zaidi.
Akiongea na CGTN mtaalamu huyu amesema hatua hii itaongeza imani zaidi ya wawekezaji wa kigeni na kuhimiza uwekezaji zaidi katika sekta ya utengenezaji ya China. Anaona kuwa sera hii imekuja kwasababu kwa sasa uvutiaji wa uwekezaji wa moja kwa moja wa China umeanza kuwa na changamoto, na hii ni inatokana na sababu za msingi za kiuchumi. Hivyo amesema China inataka kupambana na hali ya mpito kwa kutambulisha kidogo kidogo hatua hizi ili kuvutia zaidi uwekezaji wa moja kwa moja.
Akitolea mfano wa tangazo la kiwanda cha betri lilitolewa miezi miwili iliyopita, na kiongozi mwenye ushawishi katika jamii ya wafanyabishara wa magharibi Bw. Gong amesema taarifa hii ni kubwa. Mfanyabiashara huyo wa kutengeza betri ambaye amefanya uwekezaji mkubwa huko Shanghai, betri zake sio tu zitakuwa ni kwa ajili ya gari zake bali pia kwa sekta ya nishati, kwa mfano gridi za umeme.