UM walaani mauaji ya raia 468 yaliyofanywa na wanamgambo nchini Sudan Kusini
2024-07-18 09:01:22| CRI

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) Jumatano ilieleza wasiwasi juu ya kuenea kwa mashambulizi dhidi ya raia yanayofanywa na makundi ya wanamgambo ya kijamii nchini humo.

UNMISS ilisema kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu wa 2024, imerikodi matukio 240 ya vurugu, ambayo yamewaathiri raia 913 kote nchini, watu 468 kati yao waliuawa, watu 328 kujeruhiwa, na wengine 70 walitekwa nyara, huku 47 wakikumbwa na ukatili wa kijinsia, ikionesha asilimia 24 ya ongezeko la idadi ya matukio ya vurugu ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo.

UNMISS ilitoa ripoti mjini Juba ikisema vurugu ndani ya jamii zilizofanywa na wanamgambo wa kijamii au makundi ya ulinzi wa raia ni chanzo cha msingi cha vurugu nchini humo, ambapo kwa jumla asilimia 87 ya wahanga walirikodiwa nchini humo kutokana na vurugu hizo.