Afisa wa Zambia aipongeza China kwa mpango wa mafunzo ya utawala bora
2024-07-18 09:00:01| CRI

Afisa mwandamizi wa serikali ya Zambia Jumatano aliipongeza China kwa kutoa mafunzo ya kina katika kujenga uwezo wa utawala bora na mipango ya uchumi mkuu kwa maafisa waandamizi wa serikali ya Zambia.

Waziri wa Jimbo la Copperbelt, Elisha Matambo, ambaye alikuwa miongoni mwa mawaziri na makatibu wakuu waliopata mafunzo haya hivi karibuni nchini China, alitoa shukrani kwa serikali ya China kwa kuandaa mpango huo. Alisema viongozi hao watatumia elimu kubwa waliyopata wakati wa mafunzo hayo ili kuboresha utoaji huduma katika idara mbalimbali za serikali na mikoa.

Aidha alisema viongozi hao walipewa fursa ya kupata uzoefu wa moja kwa moja kwa kutembelea mashirika mbalimbali ya China kama Huawei na PowerChina ili kuelewa zaidi shughuli zao. Alisisitiza kuwa Zambia inapenda kushirikiana na serikali ya China na kujifunza kutokana na uzoefu wake ili kuboresha maisha ya watu wake.