Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF), ambalo pia linajulikana kama Tamasha la Nchi za Jahazi, litakuwa na filamu zaidi ya 3,000 kutoka kote duniani.
Hayo yamesemwa na afisa mkuu mtendaji wa ZIFF Joseph Mwale kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika Jumanne jijini Dar es Salaam. Amesema tamasha hilo ambalo ni tukio kubwa la kitamaduni la Zanzibar litakalofanyika Agosti 1 hadi 4, litawavutia watengeneza filamu kutoka nchi 100, zikiwemo China, Tanzania, Ujerumani, Uingereza, Indonesia, Poland, Argentina, Hispania, Brazil, Marekani na nchi nyingine za Afrika.
Tamasha hilo litakalo jumuisha shughuli kama vile maonesho ya filamu na mashindano, warsha, sanaa na maonesho, na kuvutia zaidi ya wageni 200,000 duniani, linalenga kuendeleza na kutangaza tasnia ya filamu na za utamaduni kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa kikanda.