Zimbabwe kuandaa maonyesho ya kwanza ya uwekezaji kutoka China
2024-07-19 23:15:38| cri

Zimbabwe inapanga kufanya maonyesho ya kwanza ya uwekezaji kutoka China baadaye mwaka huu ili kuonyesha uwekezaji wa China katika sekta mbalimbali na mchango wake katika uchumi wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kilimo katika Shirikisho la Kilimo la Zimbabwe Maxwell Mutema amesema, baadhi ya kampuni za China zimethibitisha kushiriki katika maonyesho yajayo ya kilimo ya Zimbabwe yaliyopangwa kuanza Agosti 26 hadi 31 mjini Harare.

Mutema amesema maonyesho hayo yatakuwa ni maalum kuonyesha umuhimu wa uwekezaji wa China katika kilimo na sekta nyingine mbalimbali nchini Zimbabwe katika miaka iliyopita.