EAC na washirika wa IOM kuimarisha usalama wa afya katika mipaka ya kanda
2024-07-19 09:06:49| CRI

Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imesema kwamba inashirikiana na Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) ili kuimarisha usalama wa afya wa kuvuka mipaka na kukabiliana na milipuko ya magonjwa katika maeneo ya mipakani.

EAC imetoa taarifa kwamba Kanda ya Afrika Mashariki yenye wakazi zaidi ya milioni 300, imeathiriwa na masuala ya usalama wa afya wa kuvuka mipaka na milipuko ya magonjwa kama vile kipindupindu, ebola, na janga la COVID-19 katika miaka michache iliyopita. Katika baadhi ya nchi, milipuko hii imesababisha kuvunjika kabisa kwa mifumo ya afya ya umma, ambayo imeelemewa na kushindwa kuikabili.

Afisa mkuu wa afya wa EAC Eric Nzeyimana amesema kuwa EAC imeazimia kuwa na mawasiliano thabiti ya hatari na mkakati wa ushirikishwaji wa jamii ili kusimamia kwa ufanisi na kupunguza hatari zinazohusiana na dharura za afya ya umma na majanga mengine ya kiafya.