Rais Xi Jinping wa China ametoa maelezo kuhusu azimio la Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) la kuendeleza zaidi mageuzi kwa kina ili kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa kwa umaalumu wa China.
Rais Xi amesema, azimio hilo limetolewa kwa lengo la kutimiza kwa kimsingi mambo ya kisasa kwa umaalumu wa China ifikapo mwaka 2035, likiweka mipango kuhusu hatua kuu za mageuzi zitakazotekelezwa katika miaka mitano ijayo. Amesema azimio hilo linazingatia jukumu la kuongoza mageuzi ya muundo wa kiuchumi, ujenzi wa utaratibu unaosaidia uvumbuzi kwa pande zote, mageuzi ya kina, kujumuisha maendeleo na usalama, na kuimarisha uongozi wa Chama katika mchakato wa mageuzi.
Pia amesema anatumaini kuwa wajumbe wote wataelewa kwa kina moyo wa Kamati Kuu ya CPC, kufanya majadiliano juu ya mada hiyo na kutoa maoni na mapendekezo ya kiujenzi, ili kurekebisha vizuri rasimu ya azimio hilo.