Meli ya “upinde wa amani’ ya Jeshi la China yatoa huduma za matibabu ya bure kwa watanzania.
2024-07-22 14:43:26| cri

Meli ya Jeshi la Wanamaji la Jeshi la Ukombozi la Umma la China iliyotia nanga katika bandari ya Dar es Salaam Julai 16 na kuendelea kuwepo hadi Julai 23, 2024, imetoa fursa nzuri kwa Watanzania kupata huduma za matibabu bure, na kupokea idadi kubwa ya watu wanaohitaji huduma.

Meli hiyo imekwenda Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango wa maadhimisho ya miaka 60 ya jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Maelfu ya Watanzania, hasa wenye matatizo ya afya na wenye changamoto za kiuchumi, wengine wakiwa wamepoteza kabisa matumaini ya kupata matibabu kutokana na kukosa fedha, wamemiminika kwenye meli hiyo kupata nafasi ya kupewa huduma za matibabu.