Kiongozi wa Nigeria atoa salamu za rambirambi kwa Vietnam kufuatia kifo cha Nguyen Phu Trong
2024-07-22 14:47:30| cri

Rais Bola Tinubu wa Nigeria ametoa salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Vietnam kufuatia kifo cha Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) Nguyen Phu Trong.

Kwenye salamu zake za rambirambi, Rais Tinubu amewahakikishia watu wa Vietnam kuwa Nigeria itaungana mkono na Vietnam katika kipindi hiki cha huzuni, huku akieleza kusikitishwa kwake na kifo cha Nguyen Phu Trong. Pia amepongeza mchango mkubwa na juhudi kubwa za kiongozi huyo katika kuiendeleza Vietnam.