Wawekezaji wa EAC wapiga hatua kubwa katika kuingia kwenye soko la Kenya
2024-07-22 22:42:52| cri

Makampuni ya eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yanazidi kuongezeka na kupanua shughuli zao katika sekta muhimu za Kenya, ikiwa ni pamoja na huduma, viwanda, kilimo mafuta na gesi, na kubadili mwelekeo wa zamani ambapo Makampuni ya Kenya kwa muda mrefu yamekuwa yakitawala masoko ya eneo hilo .

Wawekezaji kutoka Uganda, Tanzania, Rwanda na Somalia wamekuwa wakipanua shughuli zao nchini Kenya, na kuleta ushindani ambao haukuwepo kwa miaka mingi ambapo Kampuni za Kenya, zikiwemo benki, bima na viwanda zilikuwa zikijitanua katika soko la Afrika Mashariki kutafuta fursa mpya.