Sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ni ufunguo wa kutimiza mambo ya kisasa
2024-07-22 08:28:50| cri

Mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefanyika na kufungua ukurasa mpya wa kuhimiza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango nchini China. Rais Xi Jinping amesisitiza kwamba mageuzi na ufunguaji mlango ni ufunguo wa kutimiza mambo ya kisasa kwa njia ya Kichina.

Mkutano huo ulipitisha Uamuzi wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China juu ya Kukuza zaidi Mageuzi, ili Kuhimiza Utimiaji wa Mambo ya Kisasa kwa Njia ya Kichina. Uamuzi huo umechambua hali mpya na changamoto mpya zinazokabili utumiaji wa mambo ya kisasa nchini China, na kutoa mpangilio wa kukuza mageuzi kwa pande zote.

Mageuzi huendana na ufunguaji mlango. Ufunguaji mlango ni ishara dhahiri ya mambo ya kisasa ya Kichina. Uamuzi huo umesema China itaongeza uwezo wa kufungua mlango wakati ikipanua ushirikiano wa kimataifa, kujenga mfumo mpya wa kiuchumi, kukuza mageuzi ya mifumo ya usimamizi wa uwekezaji wa kiegni nchini China na uwekezaji wa China kwa nchi za nje, na kukamilisha na kuhimiza mfumo wa ujenzi wa pamoja wa ngazi ya juu wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Mhariri mtendaji wa gazeti la Nipashe Betreace Bandawe alisema kuwa amefurahi sana kuona kuwa chini ya uongozi wa Rais Xi, China inachukua hatua za kivitendo kusaidia maendeleo ya kijani barani Afrika, Tanzania na Afrika zinaichukulia China kama mshirika muhimu wa ushirikiano anayetegemewa. Na kuwa China siku zote imekuwa mbele katika kuwekeza katika nchi nyingine zinazoendelea, na Tanzania na nchi nyingine za Afrika zinatarajia kupanua zaidi ushirikiano na China.

Mwenyekiti wa Kituo cha Utafiti wa Kiswahili cha Mwalimu Nyerere Profesa Aldin Kai Mutembei amesema mafanikio ya kiuchumi ya China ni ushahidi bora wa mafanikio ya mageuzi na kufungua mlango. China imeithibitishia dunia mafanikio ya mfumo wa ujamaa wenye umaalum wa China kupitia maendeleo yake ya kijamii na kiuchumi. Amesisitiza kuwa ujenzi wa mfumo wa demokrasia na mtindo wa usimamizi wa jamii pia ni mfano wa kuigwa kwa nchi za Afrika.

Mhadhiri wa uchumi na mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Humphrey Moshi alisema utaratibu wa ushirikiano kati ya China na nchi zinazoendelea ni chachu muhimu ya kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi hizo. Tofauti na nchi za Magharibi, China inaheshimu matakwa ya kila nchi ya Afrika na ina vipaumbele tofauti katika ushirikiano na nchi tofauti. Ushirikiano kati ya China na Afrika umejengwa kwenye mazungumzo na unaonyesha sifa za kuheshimiana na usawa. Ametoa wito kwa China na Afrika kuanzisha mfumo wa kufunga mahesabu za kifedha na kibiashara kwa kutumia sarafu ya RMB, na pia anatumai kuwa China itahimiza maendeleo ya sekta ya nishati mpya barani Afrika.

Mkuu wa kituo cha televisheni cha Star TV cha Tanzania Steve Diallo alieleza kuwa China ni mshirika mkuu wa biashara wa Afrika, na mtindo wa maendeleo ya uchumi wa China kupitia mageuzi na ufunguaji mlango ni mfano wa kuigwa kwa Tanzania. Kwa sasa, ushirikiano kati ya China na Tanzania umejikita zaidi katika miundombinu, kilimo, madini na biashara, na anatarajia kuwa nchi hizo mbili zinaweza kuimarisha ushirikiano na mawasiliano kati ya vyombo vya habari katika siku zijazo.

Mwakilishi wa mkurugenzi mtendaji wa Africa Media Group Augustino Mganga katika hotuba yake kwanza amepongeza kufanyika kwa mafanikio kwa Mkutano wa Tatu wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC. Alisema, "nimesoma baadhi ya vitabu kuhusu fikra za Rais Xi Jinping, na nakubaliana sana na pendekezo la Rais Xi la kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Mkakati wa utawala wa nchi wa Rais Xi Jinping unaielekeza China kuboresha sifa ya uchumi wake kupitia uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, na pia kuwezesha bidhaa za teknolojia ya juu na huduma za China kunufaisha nchi nyingine. Chini ya uongozi wa rais Xi, mawasiliano ya kitamaduni yanayoimarika kati ya China na Tanzania yamewawezesha watu wa Tanzania kunufaika na maendeleo ya kisasa ya China.”