AU na BADEA zaanzisha uhusiano wa kiwenzi ili kuhimiza maendeleo ya Afrika
2024-07-22 14:50:26| cri

Umoja wa Afrika na Benki ya Kiarabu kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika BADEA jana pembezoni mwa Mkutano wa 6 wa uratibu wa nusu mwaka wa AU unaofanyika mjini Accra, Ghana, walizindua muungano wa mambo ya fedha wa nchi za kiarabu na Afrika, ili kuhimiza utafutaji wa fedha kwa ajili ya maendeleo ya Afrika.

Rais Nana Akufo-Addo wa Ghana amesema, kuanzisha uhusiano thabiti wa kiwenzi kati ya nchi za Afrika na za kiarabu ni hatua ya kuelekea mwelekeo sahihi wa maendeleo kwa pamoja.

Pia ameisifu BADEA kwa kuunga mkono maendeleo ya Afrika katika miaka 50 iliyopita, na unyumbufu wake mkubwa na uwezo wake wa kujibu katika kukabiliana changamoto za maendeleo ya Afrika.