Rais wa Kenya aonya dhidi ya maandamano yenye vurugu
2024-07-22 08:29:17| CRI

Rais wa Kenya William Ruto ameahidi kuwa serikali yake haitaruhusu maandamano yenye vurugu ambayo yamesababisha usumbufu mkubwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Akizungumza katika Kaunti ya Bomet, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, Rais Ruto amesema serikali itachukua hatua kali ili kulinda maisha ya watu na mali za Wakenya wote, na kuuhakikishia umma wa nchi hiyo kuwa hatua kali za kiusalama zimechukuliwa ili kuhakikisha hakuna kundi linalotishia amani iliyopo sasa nchini humo.

Pia rais Ruto amesema ametoa mwaliko kwa kila mmoja, na kuwatia oyo waandamanaji vijana maarufu kama Gen-Z kueleza madai yao kufuatia maandamano makubwa yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 50 na wengine wengi kujeruhiwa, pamoja na uharibifu wa mali nchini humo.

Rais Ruto amesema, wakati umefika kwa kundi hilo lisilo na kiongozi wala muundo, kuwasilisha ajenda yao mbadala badala ya kujihusisha na maandamano yanayosababisha uharibifu mkubwa.