Kenya yalenga kuwawezesha vijana kwa sayansi, teknolojia ili kuchochea maendeleo
2024-07-23 14:33:33| cri

Wizara ya Elimu ya Kenya imesema inadhamiria kutumia sayansi, teknolojia na uvumbuzi ili kuwawezesha vijana na kuchochea maendeleo nchini humo.

Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu Beatrice Inyangala amesema serikali inatoa kipaumbele kwa utafiti na ubunifu ili kutatua changamoto nyingi za kijamii. Amesema serikali imeanza ushirikiano na washirika wa ndani na kimataifa ili kuendeleza ubora wa utafiti katika taasisi zote za elimu. Bibi Inyangala amesema hayo wakati wa kongamano la ushiriki wa wadau wa tamasha la utafiti huko mjini Nairobi.

Ameongeza kuwa Kenya inajifunza uzoefu mzuri kutoka nchi za China, Korea Kusini, Malaysia na Singapore, ili kuchochea ukuaji wa nchi hiyo kwa njia ya kisayansi na uvumbuzi.