Kagame anasema Rwanda iliyojengwa kwa umoja, itathamini amani na usalama
2024-07-23 23:19:52| cri

Rais mteule Paul Kagame, Mwenyekiti wa chama RPF-Inkotanyi, amesisitiza kuwa Rwanda imejengwa na umoja wa watu wake baada ya historia mbaya iliyoiharibu nchi hiyo, na sasa ni rafiki wa kutegemewa na nchi nyingine. Rais Kagame amesema Rwanda ni rafiki wa kutegemewa lakini kama ikichukuliwa kuwa adui licha ya juhudi zake zote zinazolenga ushirikiano, haitakaa kimya kulinda amani na usalama wake.

Rais Kagame amesema hayo wakati wa tafrija iliyohudhuriwa na wanachama wa RPF-Inkotanyi na vyama washirika kisiasa, wasanii, watu kutoka sekta binafsi, na wanachama wa mashirika ya kiraia. Ameishukuru familia yake, uongozi na wanachama wa RPF, vyombo vya usalama, sekta binafsi, na wengine wengi kwa msaada wao katika kipindi chote cha kampeni na uchaguzi.