Baraza la ASEAN na AFRIKA kuangazia uwezo muhimu wa madini wa Tanzania
2024-07-23 14:21:20| cri

Tanzania inatarajiwa kunufaika na Baraza la Uwekezaji wa Madini la ASEAN na AFREIKA (AAMIF) kupitia fursa ya kuonyesha uwezo wake wa madini ikiwa ni pamoja na kumiliki hazina kubwa ya madini muhimu.

Baraza hilo linalotarajiwa kufanyika Bangkok, Thailand, mwishoni mwa mwaka huu, linalenga kukuza raslimali muhimu za madini kwa kuvutia ushirikiano na kuhimiza kuanzishwa kwa viwanda vya kuongeza thamani na utengenezaji bidhaa katika nchi za Afrika. Baraza hilo linatarajiwa kuvutia zaidi ya nchi 30 za Afrika, pamoja na wawekezaji na wafadhili kote duniani.

Baraza hilo linatazamia kutoa fursa muhimu kwa nchi za ASEAN na Afrika kuimarisha sekta za madini na kuunda ushirikiano wa kimkakati, ambao unaweza kusukuma ukuaji endelevu wa uchumi na maendeleo.