Ufikiaji wa huduma ya 5G kwa Tanzania yapanuka kwa kasi na kufikia asilimia 15
2024-07-23 14:16:06| cri

Asilimia ya idadi ya watu wa Tanzania wanaofikiwa na huduma ya mawasiliano ya habari ya kizazi cha tano (5G) imepanda hadi kufikia asilimia 15 katika robo ya pili ya mwaka huu wa kalenda, kutokana na uwekezaji unaoendelea katika miundombinu ya mawasiliano nchini Tanzania.

Ripoti mpya ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaonyesha kuwa mawasiliano ya 5G yamepanda kutoka asilimia 13 ya watu katika robo ya kwanza hadi asilimia 15 katika robo ya pili. Tanzania ilizindua huduma ya 5G mwaka jana. Ufikiaji wa 3G umefikia asilimia 89 ya idadi ya watu, na hivyo kuimarisha upatikanaji wa huduma za data, wakati ufikiaji wa 4G umefikia asilimia 83, hali ambayo imeboresha kasi na uaminifu wa mtandao.