Watu 20 wafariki kufuatia maporomoko ya ardhi kusini mwa Ethiopia
2024-07-23 08:36:21| CRI

Vyombo vya habari vya Ethiopia vimeripoti kuwa, watu takriban 20 wamefariki kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyotokea kusini mwa nchi hiyo.

Shirika la Utangazaji la nchini humo Fana limeripoti kuwa, maporomoko yalitokea Jumatatu saa nne asubuhi kwa saa za huko, katika Wilaya ya Geze Gofa.

Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Misikir Mitiku amesema hadi sasa waokoaji wamepata miili zaidi ya 20 iliyofukiwa chini ya matope.

Pia amesema idadi ya vifo huenda itaongezeka wakati shughuli za uokoaji zikiendelea.