Afrika Kusini yalenga kuhimiza biashara kupitia jukwaa la BRICS
2024-07-23 14:32:54| cri

Naibu waziri wa biashara, viwanda na ushindani wa Afrika Kusini Zuko Godlimpi jana amesema, nchi yake itahudhuria mkutano wa mawaziri wa biashara wa nchi za BRICS utakaofanyika mjini Moscow, Russia, ili kutafuta fursa ya biashara na uwekezaji.

Godlimpi amesema, Afrika Kusini itaendelea kutafuta fursa za ushirikiano na nchi za BRICS, pamoja na ushirikiano wa pande mbili na ushirikiano kupitia jukwaa la BRICS, ambao utatoa fursa kwa bara la Afrika kubadilisha jukumu lake la kuuza bidhaa na kuwa bidhaa zenye ongezeko la juu la thamani.