Idara ya Afya ya Ukanda wa Gaza wa Palestina imesema watu 70 wameuawa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa katika shambulio la bomu lililofanywa na jeshi la Israel dhidi ya mji wa Khan Younis ulioko Ukanda wa Gaza.
Kulingana na ripoti ya Shirika la Habari la Palestina jana, ndege nyingi za kivita za Israel zilishambulia mji huo, na kwamba kabla ya shambulizi hilo, idadi kubwa ya wakazi wa eneo hilo walihamishiwa sehemu ya magharibi. Hata hivyo bado kuna watu wengi waliouawa katika mashambulizi kutokana na muda wa kuwahamisha kuwa mdogo.
Jeshi la Ulinzi la Israel lilitoa taarifa jana na kusema kwamba, liliwataka watu wa mji wa Khan Yunis kuondoka mapema kwa kuwa taarifa za kijasusi zilionyesha kuwa "magaidi" wanaendesha shughuli zao kutokea maeneo hayo.