Kenya imepokea mabehewa 20 mapya ya abiria kutoka China, ili kuongeza uwezo wake wa usafirishaji na kuboresha uzoefu wa abiria.
Mabehewa hayo ni pamoja na mabehewa 10 ya daraja la pili, mabehewa manne ya daraja la juu, behewa moja la mgahawa, behewa moja la nishati, na mabehewa manne ya daraja la kwanza.
Katibu wa kwanza wa Wizara ya barabara na usafirishaji wa Kenya Mohamed Daghar amesema, hii ni hatua muhimu kwa wizara yake, kwani wataendelea kuboresha ufanisi wa uendeshaji na utoaji wa huduma katika idara za usafirishaji.