Rais Kagame ashinda tena katika uchaguzi wa urais nchini Rwanda
2024-07-23 08:47:59| cri



Tume ya Uchaguzi ya Rwanda jana ilitangaza matokeo rasmi ya uchaguzi wa urasi, ambapo rais wa sasa wa nchi hiyo Paul Kagame alipata ushindi na ataendelea na wadhifa huo.

Takwimu zilizotolewa na tume hiyo zimeonesha kuwa, rais Kagame alipata kura zaidi ya milioni 8.8, ambazo zilichukua asilimia 99.18.

Mwezi Aprili mwaka 2000, Kagame aliteuliwa kuwa rais wa Rwanda katika Mkutano wa pamoja wa bunge na baraza la mawaziri, na mwezi Agosti mwaka 2003, alipata ushindi kwenye uchaguzi wa urais ulioshirikisha kwa mara ya kwanza vyama vingi vya siasa. Kwenye uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka 2017, Kagame alipata ushindi kwa mara nyingine.