Kenya kuvutia wawekezaji wa China katika bustani ya kijani ya viwanda
2024-07-23 08:37:37| CRI

Kenya inajizatiti kuvutia wawekezaji kutoka China kuanzisha shughuli zao katika bustani ya kijani ya viwanda iliyoko Naivasha, umbali mfupi kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi.

Katibu mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda nchini Kenya, Abubakar Hassan Abubakar ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua jijini Nairobi, kuwa bustani hiyo iko katika eneo lenye joto kutoka ardhini, ambalo ni chanzo endelevu na cha kudumu cha nishati.

Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa uwekezaji wa China katika sekta za uchumi wa kijani, ikiwemo viwanda vya umeme wa jua na urejelezaji.