Rais wa China ampongeza rais Kagame kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Rwanda
2024-07-24 08:33:37| cri



Rais Xi Jinping wa China jana alimpigia simu rais Paul Kagame wa Rwanda na kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo.

Rais Xi amesema, Rwanda ni nchi rafiki wa China, na katika miaka kadhaa iliyopita, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepata maendeleo ya kasi, na kupata mafanikio mengi kwenye ushirikiano wa sekta mbalimbali, urafiki wa jadi kati yao pia umezidishwa zaidi.

Rais Xi amesema anapenda kushirikiana na rais Kagame kukuza zaidi uaminifu wa siasa, kupanua zaidi ushirikiano wa ufanisi, na kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.