Nigeria yalaani vitendo vya kibaguzi vya Meta ikiitoza faini ya dola milioni 220 za kimarekani
2024-07-24 11:18:32| cri

Mamlaka ya usimamizi wa ushindani ya Nigeria imesema kampuni za teknolojia za Marekani Meta Platforms na WhatsApp zimetozwa faini ya dola milioni 220 za kimarekani na Nigeria hivi karibuni kutokana na vitendo vya kibaguzi na makosa yanayostahili kuwekewa vikwazo.

Kamati ya ushindani na kulinda watumiaji ya Nigeria (FCCPC) ilifanya mkutano na wanahabari mjini Abuja ikisema kampuni hizo zimeadhibiwa vikali baada ya uchunguzi wa kina uliochukua miaka mitatu.

Kaimu mkurugenzi wa FCCPC Adamu Abdullahi alisema Meta Platforms imekutwa na hatia ya kuzinyima kampuni ya Nigeira haki ya kujiamulia, kufanya miamala isiyoidhinishwa, na kutoa data binafsi.