China yasema nchi zenye silaha za nyuklia zinapaswa kusaini mkataba au kutoa tamko la kisiasa kuhusu matumizi ya silaha hizo
2024-07-24 08:31:44| cri

Mkutano wa pili wa maandalizi ya Mkutano wa Kumi na Moja wa Mapitio ya Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia ulifanyika jumatatu wiki hii huko Geneva, Uswisi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesema, China ikiwa nchi iliyosaini mkataba huo, imekuwa ikishikilia kwa uthabiti kanuni na madhumuni ya mkataba huo, kutekeleza kwa uaminifu wajibu wake chini ya mkataba huo, na kuhimiza uendelezwaji wa kina na kwa uwiano nguzo tatu za kuondoa silaha za nyuklia, kutoeneza silaha hizo na matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia.

Bibi Mao pia amesema, China itafuata kimsingi pendekezo la Rais wa nchi hiyo Xi Jinping la kuzingatia dhana ya usalama wa pamoja, shirikishi na endelevu, kufanya kazi bega kwa bega na pande zote, na kukuza kwa pamoja amani ya dunia, usalama na maendeleo.

Katika mkutano huo, China iliwasilisha nyaraka nne za kazi kuhusu mpango wa kila upande kutotangulia kutumia silaha za nyuklia, usalama usio wa nyuklia, udhibiti wa silaha za nyuklia, na ushirikiano wa nyambizi za nyuklia kati ya Marekani, Uingereza na Australia.