Idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya ardhi nchini Ethiopia yafikia 229
2024-07-24 08:35:04| CRI

Idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya ardhi kusini mwa Ethiopia imeongezeka na kufikia 229.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Serikali ya Ukanda wa Gofa imesema, watu waliofariki kutokana na maporomoko hayo yaliyotokea jumatatu saa nne asubuhi kwa saa za huko katika wilaya ya Geze Gofa ni pamoja na wanaume 148 na wanawake 81.

Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Ethiopia na wataalamu kutoka maeneo ya jirani wako katika eneo la tukio kuwasaidia waathirika wa janga hilo.

Janga hilo limetokea wakati Ethiopia ikiwa katikati ya msimu wa mvua, ambao ulianza Julai na unatarajiwa kuendelea mpaka katikati ya mwezi Septemba.