Watu 26 wauawa katika shambulio lililofanywa na kundi la kigaidi nchini Mali
2024-07-24 08:34:34| CRI

Watu 26 wameuawa kufuatia shambulio lililofanywa na kundi la kigaidi katika kijiji cha Dembo kilichoko katikati ya Mali.

Ofisa wa huko ambaye hakutaka kutaja jina lake ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, shambulio hilo limefanywa dhidi ya wanakijiji waliokuwa wakiendelea na shughuli za kilimo.

Katika miezi ya karibuni, mashambulio dhidi ya raia yameongezeka katika eneo la katikati ya Mali, ambapo Julai Mosi, makundi ya kigaidi yaliyokuwa na silaha yalishambulia vijiji vya Djiguibombo na Sokorokanda na kusababisha vifo vya watu 23.