Kuongezeka kwa simu za mkononi barani Afrika kwaongeza uanaharakati wa kidijitali
2024-07-24 11:16:56| cri

Kuongezeka kwa matumizi ya simu za mkononi katika bara zima la Afrika, kimehimiza matumizi ya simu za mkononi kutoka kwenye matumizi ya kawaida ya simu kama vile kupiga simu, hadi kwenye kushiriki katika miamala ya biashara ya mtandaoni.

Ripoti tatu tofauti zinaonyesha kuwa bara la Afrika linashuhudia mabadiliko makubwa ya kasi ya matumizi ya vifaa vya mkononi vinavyotumia mtandao wa internet, vinavyoweza kupiga picha bora na kuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi data, kutokana na 'kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za kidijitali na ushiriki wa mitandao ya kijamii'.

Shirika la Kimataifa la Data (IDC) linaonyesha kuwa katika robo ya kwanza ya 2024, usafirishaji wa simu za mkononi barani Afrika uliongezeka kwa asilimia 17.9 na kufikia simu milioni 20.2 ikilinganishwa na mwaka uliopita.