Umoja wa Mataifa wasema watu milioni 733 walikabiliwa na njaa duniani mwaka 2023
2024-07-25 08:53:47| cri



Ripoti ya mwaka 2024 ya "Hali ya Usalama wa Chakula na Lishe Duniani" iliyotolewa jana kwa pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Afya Duniani (WHO) imesema, mwaka jana, takriban watu milioni 733 ulimwenguni kote walikabiliwa na njaa, na mtu 1 kati ya 11 halikuwa na chakula cha kutosha. 

Ripoti hiyo imesema, kasi ya kimataifa ya kutokomeza njaa haiendelei bali inarudi nyuma, na kiwango cha utapiamlo ni sawa na kile kilichokuwepo miaka 15 iliyopita.