China yatuma salamu za rambirambi kwa Ethiopia kwa maafa makubwa yaliyotokana na maporomoko ya ardhi
2024-07-25 08:41:41| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesema China inatuma salamu za rambirambi kwa watu walioathiriwa na maporomoko makubwa ya ardhi yaliyotokea nchini Ethiopia hivi karibuni na kusababisha hasara kubwa.

Habari zinasema, maporomoko ya ardhi yalitokea hivi karibuni katika eneo la Geze Gofa, kusini mwa Ethiopia na kusababisha vifo vya watu 229, idadi ambayo huenda ikaongezeka zaidi.