Rais wa Jamhuri ya Congo asema nchi hiyo iko tayari kushirikiana na China kukuza ushirikiano wa kiutendaji
2024-07-25 08:41:13| CRI

Rais wa Jamhuri ya Congo Denis Sassou-Nguesso amesema, nchi yake iko tayari kushirikiana na China kuimarisha kuaminiana kisiasa, kuhimiza ushirikiano wa kiutendaji, na kuhimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili katika kiwango cha juu zaidi.

Rais Sassou Nguesso amesema hayo alipokutana na mwakilishi maalumu wa serikali ya China kuhusu masuala ya Afrika Bw. Liu Yuxi huko Brazzaville, mji mkuu wa nchi hiyo. Pia amesema nchi yake inathamini urafiki wa jadi na China, na kwamba inatarajia kuhudhuria mkutano wa ujao wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika mwaka huu, ambao pia ni mwaka wa 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Bw. Liu Yuxi amesema, China inapenda kutumia fursa ya mkutano ujao wa FOCAC, kukuza ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali, ili kukaribisha Maadhimisho ya Miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.