Tume cha uchaguzi ya Rwanda imetangaza kuwa idadi ya wabunge wanawake kwenye baraza la chini la Bunge la Rwanda imeongezeka na kuwa asilimia 63.8 ya wajumbe 80 wa Baraza hilo, wakiongezeka kutoka asilimia 61 katika bunge lililopita.
Ripoti ya mwaka 2021 iliyopewa jina la ‘Wanawake Bungeni’ iliyochapishwa na Muungano wa Mabunge ya Duniani ilionyesha kuwa Rwanda ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya wanawake katika nyadhifa serikalini. Mbali na asilimia 63.8 ya wabunge hao, viti 13 vya uwaziri kati ya 32 vilivyopo katika baraza la mawaziri la sasa vinakaliwa na wanawake.
Miongoni mwa wabunge wanawake katika bunge jipya wale waliokuwepo, akiwemo Christine Bakundifite aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), inayoongoza uchunguzi wa taasisi na viongozi wa serikali.