Idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya ardhi nchini Ethiopia huenda ikafikia 500
2024-07-26 08:54:00| CRI

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (UNOCHA) jana imeonya kuwa huenda idadi ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya ardhi kusini mwa Ethiopia inaweza kufikia 500.

Katika ripoti yake kuhusu hali ya sasa iliyotolewa jana na kunukuu mamlaka za huko, OCHA imesema idadi ya vifo imeongezeka na kufikia 257 mpaka jumatano, na miili mingine inazidi kutolewa kutoka kwenye tope.

Kwa mujibu wa mamlaka za huko, maporomoko ya kwanza yalitokea jumapili usiku baada mvua kubwa kunyesha katika kijiji kidogo cha Kencho Shacha Gozdi, wilaya ya Geze Gofa kusini mwa Ethiopia, na maporomoko ya pili yalitokea jumatatu asubuhi na kufukia idadi isiyojulikana ya watu wa huko waliokusanyika katika sehemu ya kwanza ya maporomoko ili kusaidia juhudi za uokoaji.