Jeshi la China kushiriki kwenye luteka ya pamoja barani Afrika, na nchini Mongolia
2024-07-26 14:19:55| cri

Wanajeshi wa China, Tanzania na Msumbiji watafanya luteka ya pamoja ya "Peace Unity-2024" kuanzia mwishoni mwa Julai hadi katikati ya Agosti barani Afrika.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Zhang Xiaogang amesema luteka hiyo itashuhudia wanajeshi wakiendesha operesheni za pamoja za kijeshi za kukabiliana na ugaidi ardhini na baharini. Lengo ni kuimarisha uaminifu wa kijeshi na ushirikiano wa kivitendo ili kulinda kwa pamoja amani na utulivu wa kikanda.

Aidha kutokana na mwaliko wa Wizara ya Ulinzi ya Mongolia, kikosi cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) pia kitaenda nchini Mongolia kushiriki kwenye luteka ya kulinda amani kimataifa ya "Khaan Quest-2024" mwishoni mwa Julai.