Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ahimiza hatua za kimataifa za kukabiliana na joto kali
2024-07-26 09:00:36| cri



Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana ameitaka jumuiya ya kimataifa ichukue hatua za haraka ili kukabiliana na joto kali, kwani "joto kali si jambo la siku moja, wiki moja au mwezi mmoja." 

Bw. Guterres amesema kwamba joto kali linaongezeka duniani, na jambo hili ni hatari zaidi kwa kila mtu, kila mahali. 

Bw. Guterres amesisitiza athari za halijoto kali, akisema wimbi kubwa la joto limeikumba Sahel na idadi ya watu wanaolazwa hospitalini na vifo imeongezeka kwa kasi. Pia amesema, rekodi za joto kali zimevunjwa nchini Marekani, huku shule zikifungwa barani Asia na Afrika, na kuathiri zaidi ya watoto milioni 80.