Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa limesema boti iliyobeba wahamiaji ilipinduka katika bahari karibu na Nouakchott, mji mkuu wa Mauritania na kusababisha vifo vya watu 15 na wengine wengi hawajulikani walipo.
Taarifa iliyotolewa jumatano na Shirika hilo imesema, boti hiyo iliyokuwa imebeba wahamiaji 300 iliondoka Gambia wiki moja iliyopita na kuzama katika bahari ya Atlantiki karibu na mji wa Nouakchott jumatatu wiki hii. Walinzi wa Pwani ya Mauritania waliwaokoa watu 120 na 10 kati yao walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Mpaka sasa, wafanyakazi wa uokoaji bado wanatafuta watu ambao hawajulikani walipo.