Maofisa wa Afrika wanaohudhuria Jukwaa la 7 la Watu wa China na Afrika wamesifu matokeo ya mkutano wa 3 wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katika mkutano huo unaofanyika Changsha, mkoa wa Hunan, katikati ya China, maofisa hao wamesema, ni muhimu sana kwa China na Afrika kutafuta kwa pamoja njia ya maendeleo kuelekea usasa, na kuongeza kuwa vyama vya siasa na mashirika ya kiraia katika nchi za Afrika yako tayari kuimarisha ushirikiano na China ili kusaidia kujenga jamii ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja.
Rais wa Bunge la Burundi Gelase Daniel Ndabirabe amepongeza juhudi za China katika kuipatia Afrika uzoefu mzuri, ambao umesaidia kuboresha uelewa wa watu na kuboresha maendeleo.
Zaidi ya wawakilishi 200 kutoka nchi zaidi ya 50 za Afrika wameshiriki kwenye mkutano huo ulioandaliwa kwa pamoja na Idara ya Mawasiliano na Nje ya Kamati Kuu ya CPC na Kamati ya CPC ya mkoa wa Hunan.