Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Russia Sergey Lavrov.
Bw. Wang Yi amesema, China inapenda kushirikiana na Russia kulinda muundo wa ushirikiano wa kikanda unaozingatia ASEAN, wenye uwazi na shirikishi, kusukuma mbele mfumo uliopo sasa wa Asia ya Mashariki kuzidisha ushirikiano, na kuhimiza amani, utulivu na ustawi wa kanda hiyo.
Bw. Lavrov amesema, Russia itashirikiana na China kuunga mkono hadhi ya ASEAN na kuzuia kuingiliwa na nguvu za nje.