Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imeidhinisha malengo ya reli hiyo ya kusafirisha mizigo tani laki 3.5 na abiria milioni 3.43 katika mwaka mpya wa fedha 2024/2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumamosi iliyopita na makao makuu ya TAZARA, idhini hiyo imetolewa katika mkutano wa 122 wa bodi ya wakurugenzi, ambapo bodi hiyo ikikadiria kupata mapato ya jumla ya dola za kimarekani milioni 55.19 katika mwaka huo mpya wa fedha kutoka tarehe mosi Julai mwaka huu hadi tarehe 30 mwezi Juni mwaka kesho, ambayo yanatarajiwa kupatikana kutoka pande mbalimbali ikiwemo usafirishaji wa mizigo, vifurushi, abiria, ada za ufikiaji wazi na shughuli nyingine zisizo za uendeshaji.
Pia bodi hiyo imeeleza juhudi zinazoendelea katika kufufua reli hiyo ikishirikiana na wawekezaji kutoka China.