China yapenda kuzidisha ushirikiano wa hali ya juu na IOC
2024-07-29 10:14:42| cri

Makamu wa Rais wa China Han Zheng amesema kuwa China inapenda kuzidisha na kupanua ushirikiano wa hali ya juu na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), wakati ambapo China itakuwa mwenyeji wa Michezo ya Majira ya baridi ya Asia mwaka ujao.

Bw. Han ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Rais Xi Jinping wa China ameyasema hayo alipokutana na Rais wa IOC Thomas Bach.

Han amewasilisha salamu za Rais Xi kwa Bach na kuipongeza IOC kwa kufanya sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 kwa mafanikio. Michezo ya Olimpiki inalenga kulinda amani ya dunia na kukuza umoja wa wanadamu, akibainisha kuwa Michezo ya Olimpiki ya Paris ina umuhimu mkubwa kutokana na haja ya kuendeleza Olimpiki chini ya hali ya sasa ya kimataifa. Amesisitiza kuwa China daima itaunga mkono kwa dhati maendeleo ya Michezo ya Kimataifa ya Olimpiki na imedumisha uhusiano mzuri wa muda mrefu na IOC.

Rais Bach alimwomba Han kuwasilisha salamu zake za dhati kwa Rais Xi. Amesema kuwa China daima inaunga mkono kazi za Michezo ya Olimpiki ya kimataifa, akibainisha kuwa mafanikio ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 wakati wa janga la COVID-19 ni mfano kwa nchi zote duniani wa jinsi ya kuandaa kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki.