DRC yasitisha shughuli zisizo za michezo baada ya tukio la mkanyagano wa watu kusababisha vifo
2024-07-29 08:52:08| CRI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Bw. Jacquemain Shabani, amesema kituo kikuu cha michezo cha Stadedes Martyrs kilichopo mjini Kinshasa, kitasimamisha shughuli zisizo za kimichezo, siku moja baada ya tukio la mkanyagano kusababisha vifo vya watu 9.

Sambamba na Stade des Martyrs, kituo cha Stade de Tata Raphael cha Kinshasa, pia kimewekwa kwenye orodha ya kusimamishwa hadi serikali itakapotoa taarifa nyingine. Tukio la mkanyagano lilitokea jumamosi wakati wa tamasha la mwanamuziki Mike Kalambayi, ambapo watu tisa, wakiwemo mwanamke mjamzito na watoto walifariki.