Kituo cha matibabu cha Rwanda (RBC) kimeahidi kudhibiti maambukizi ya homa ya ini aina B na aina C nchini humo kwa kuongeza juhudi za kueneza mwamko wa umma kuhusu ugonjwa huo.
Mkurugenzi wa kitengo cha magonjwa ya zinaa na magonjwa mengine yanayoambukizwa kwa njia ya damu katika RBC Bw. Janvier Serumondo, ametoa wito huo kwenye ujumbe wa kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini duniani kwa watu wa Rwanda kufanya upimaji wa hiari wa ugonjwa huo katika vituo vya afya vilivyo karibu ili kujua hali zao.
Bw. Serumondo amesema upimaji na matibabu vimegawanywa katika vituo vya afya nchini Rwanda, ambako wanyarwanda walioambukizwa na wakimbizi nchini humo wanapata huduma za matibabu bila malipo. Pia amesema wahudumu wa afya wamepewa mafunzo, na kazi za upimaji na matibabu zimeongezeka.