Rais Xi Jinping akutana na waziri mkuu wa Italia
2024-07-30 09:01:52| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana alikutana na waziri mkuu wa Italia Bibi Giorgia Meloni mjini Beijing.

Rais Xi amesema China na Italia ambazo ziko kwenye mwanzo na mwisho wa njia ya Hariri ya kale, mawasiliano ya kirafiki kati yao yaliyoendelea kwa muda mrefu, yametoa mchango mkubwa katika mabadilishano na mawasiliano kati ya staarabu za Mashariki na Magharibi, na maendeleo ya binadamu.

Rais Xi amesema moyo wa Njia ya Hariri ambao ni amani na ushirikiano, uwazi na ushirikishi, kufunzana na kunufaishana, ni hazina ya pamoja ya China na Italia.

Amesema China na Italia zinapaswa kuunga mkono na kukuza moyo wa Njia ya Hariri, kuangalia na kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili kwa mtazamo wa kihistoria, kimkakati na wa muda mrefu, na kuhimiza uhusiano huo kuendelea kwa utulivu.