Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa wasaini waraka wa ushirikiano mjini Madrid
2024-07-30 14:05:53| cri

Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa tarehe 29, Julai, wamesaini waraka wa ushirikiano mjini Madrid, Hispania, na kuafikiana kuhusu ushirikiano wa kuripoti habari za utamaduni na utalii, kutangaza chapa za utalii, na kufanya shughuli za vyombo vya habari. Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong na mkurugenzi mtendaji wa Shirika la utalii la Umoja wa Mataifa Zoritsa Urosevic wameshuhudia utiaji saini wa waraka huo.