Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na Ligi Kuu ya Soka ya Hispania La Liga Julai 29, zilitia saini waraka wa ushirikiano huko Madrid juu ya kukuza kwa pamoja mawasiliano ya sekta hiyo, kuandaa mashindano kwa pamoja, na kusaidia maendeleo ya soka ya vijana. Shen Haixiong, Naibu Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC na Mkurugenzi wa CMG, na Javier Tebas, Mwenyekiti wa La Liga walitia saini waraka huo kwa niaba ya pande zote mbili.