Mazungumzo ya "Fursa za Kimataifa Zinazotolewa na Mageuzi ya China katika Enzi Mpya" na shughuli ya mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na Hispania iliyoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG yalifanyika huko Madrid, Hispania. Wageni walioshiriki kwenye mazungumzo hayo walibadilishana maoni kuhusu fursa za maendeleo ya kimataifa zinazoletwa na China kupitia kuimarisha mageuzi kwa kina na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa kwa mtindo wa kichina, na pia kufikia makubaliano kadhaa juu ya ushirikiano katika nyanja za vyombo vya habari, filamu na televisheni, sanaa na nyinginezo.