China na Afrika zaimarisha ushirikiano wa kidigitali
2024-07-30 23:14:01| cri

Waziri wa viwanda na teknolojia ya habari wa China Bw. Jin Zhuanglong Jumatatu aliposhiriki kwenye kongamano la ushirikiano wa kidigitali kati ya China na Afrika alisema, China itaendelea kufanya ushirikiano na nchi za Afrika kwenye sekta ya kidigitali, na kuzisaidia kujenga “Afrika ya kidigitali”.

Jin alisema makampuni yataungwa mkono katika kufanya ushirikiano wa kiutendaji kwenye sekta za mawasiliano ya simu za mkononi, vituo vya data, kebo za baharini na ardhini. Pande mbili pia zitafanya juhudi katika kuhimiza maendeleo na matumizi ya teknolojia ya kidigitali.